The Tech Planner

Featured post

USALAMA APP REVIEW

Its agreeable that worst things tend to happen to us when we are alone: Be it health emergencies,  crimes etc. .All these happen to us unex...

Monday, 11 April 2016

MICHEMKO KATI YA WAPENZI WEMA SEPETU NA IDRIS SULTAN

kumetokea mihemko na michemko kati ya mshindi wa Big Brother Africa 2015 Idris Sultan na mpenzi wake wa sasa,Wema  Sepetu ,ambaye ni mpenzi wa zamani wa Diamond Platnumz

Hii ni baada ya Idris kukutana na video clip inayosambaa kwenye mitandao ikionyesha Wema Sepetu akimpa denda mwanamume mwingine.

Hata hivyo, wawili hawa bado hawajaachana ila mapenzi yao yamekumbwa na msukosuko kwani Idris,alieleza kwenye Interview moja kwamba kuona video clip ya mpenzi wake akimbusu mwanamume mwingine kumemuudhi na kumuumiza hisia zake.

Share:

Sunday, 10 April 2016

NOTI FLOW AZUNGUMZA baada ya video yake kupigwa marufuku nchini Kenya

Noti flow ambaye ni msanii wa kike kutoka nchini Kenya alizungumza kwenye Exclusive Interview na presenter Ali.

Katika interview hio iliyofanywa kwenye show ya (E-SHOW)
Noti Flow alieleza hisia zake baada ya video yake ya "SAME LOVE -inayoonyesha mapenzi ya jinsia moja" kupigwa marufuku nchini Kenya na shirika LA Kenya Films Classification Board.
Itazame interview yenyewe
HAPA

Vilevile Notiflow alifunguka wazi kuhusu hisia zake kuhusu mapenzi ya jinsia moja .Tazama

HAPA PIA

Share:

ERIC OMONDI ANAVYONUIA KUISISIMUA DUNIA NZIMA KWA UCHESHI

katika picha ambazo amepost kwenye official Instagram account yake ,mcheshi Eric Omondi aonekana kuwaandalia wakenya na dunia nzima sisimuo jingine.

Kwenye "Eric Omondi untamed 7"
Mcheshi maarufu Eric Omondi kutoka Kenya anajiandaa kwa ajili ya "world Tour " ya Kazi yake-ucheshi ,atakavyozuru dunia na kuitumbuiza hadhira yake kwa vivunja mbavu si haba.

Tarehe na siku maalumu zitawajia kwenye blogspot presenterali.blogspot.com

Share:

WILLY PAUL awapa shavu Sauti Sol kwenye kibao chake kipya

Tulimjua kwa "sitolia" "lala salama" "You never know" "Tam tam remix ft size 8"
Na vibao vikubwa ambavyo vimempandisha chati huku nchini.Willy Paul sio jina geni kwa wakenya  ha hata East Africa Kwa ujumla"

Hivi sasa msanii huyu mwenye style ya "Bongo gospel" ameachia kibao na Sauti Sol ,hit makers wa "sura yako " "Nerea" "unconditionally bae ft Ali Kiba" na vingine vingi.

Wasanii hawa wameungana katika jitihada za kuburudisha wakenya kwa Mara nyingine , na huenda kwa wakati juu wakaleta kadha mpya kwenye scene ya burudani.

Cha kufanya? Tusubiri!!!

Share:

Diamond platnumz aanzisha REALITY TV SHOW ya maisha yake


Ametuzubaisha kwa muziki na mikiki, sasa Diamond Platnumz atuduwaza kwa visiki kwenye Televisheni!!

"Muda si Mwingi Kipindi cha Maisha yangu ya kila siku, Familia na Team yangu nzima itaanza kuwa kwa Tv yako pendwa… nakuahidi sio tu eti Kireality showni Reality show Bora ambayo naamini utaipenda kunzia kwenye Quality, Mikasa na matukio yote nnayopitia mimi, Familia na Team yangu kila siku….Mengi yanaonekana, Unayoyasikia, Unayasoma ila kwenye Hiki kipindi ndio itakuwa Thibitisho la kila uvumi uusikiao….Sjui Kipini puani, Mara jicho, Mara sjui @officialshetta , Mara DNA, Mara @romyjons kutoinekana tena kwenye Tour Ghafla….Niamini mimi yote utaona na kuyapata kwa uwazi kabisa, Kaa na Mimi…….! We unavyohisi reality Show yetu itakuwa inaitwaje..? Cc @zarithebosslady @romyjons "



Ndio haya Maneno yake diamond Platnumz, star wa East Africa ,hit maker wa Make me sing, zigo remix ,nana, (the list is endless) kwenye official Instagram Handle yake. @Diamondplatnumz

Diamond Platnumz ,ambaye maisha yake yamekuwa ya kusisimua hasa kimuziki ameahidi kuwa show hii itakua Kali, yenye kusisimua na kuburudisha.Show ambayo itakua reality show Ya kwanza ya maisha ya msanii wa East Africa,kama wafanyavyo mastar wa nchi za ng'ambo,kama vile kwenye "T.I AND TINY" yake T.I ,"brotherhood " yake snoop Dogg" na "meet the Kardashians" ya Kardashian family na nyinginezo.

Kilichobaki,tungoje  vioja na burudani.

Share:

GET NOTICED

GET NOTICED
PRESENTER ALI. Powered by Blogger.

Author Details

contact us



Translate

Labels