The Tech Planner

Featured post

USALAMA APP REVIEW

Its agreeable that worst things tend to happen to us when we are alone: Be it health emergencies,  crimes etc. .All these happen to us unex...

Monday 11 April 2016

KUTANA NAYE MJUKUU WA MEYA :GWIJI KATIKA TAALUMA YA UTANGAZAJI WA REDIO

Utampata kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi ,kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne.
Kila siku akijaajaa kuijuza,kuelimisha na cha muhimu kabisa kuiburudisha hadhira yake.
Alex Muembu ni Mtangazaji mpya kwenye uwanja wa utangazaji.akitangazia K.U Radio -Mtangazaji huyu amedhihirisha tajriba na ujuzi wake wa kuchangamsha hadhira na kuipa burudani huku akiiijuza yanayotendeka kwenye maeneo ya karibu .

Mbali na utangazaji?

"Nimespecialise katika radio production,editing, na online digital marketing,nafanya vizuri sana pia katika event promotion kama Emcee" alinifafanulia.

Kwa anayoipa Hadhira yake ,nayo haimbwagi , idadi ya mazungumzo , jumbe za simu, kwenye Facebook na Twitter na SMS zinazomiminika hazina kifani.

Alipoulizwa anadhamiria kuwa kama nani?


"Napenda na kuheshimu sana kazi yake Mzazi Willy M Tuva.Mzazi amekuwa kama mwalimu kwa watangazaji wengi wachanga  ambao tumeingia kwenye sekta ya burudani hivi majuzi.Jitihada ,kipaji ,na mapenzi yake kwa muziki wa kisasa,wa Afrika mashariki ni jambo linalonivutia .support anayowapa wasanii wote,chipukizi na ambao wamekolea katika sekta hii, ni vitu vinavyovutia kwa sana." Alieleza.

Kwa wakazi wa K.U na viunga vya karibu, Utaipata K.U radio kwenye 99.9 FM .
Utampata Alex Muembu al-maarufu mjukuu wa Meya kwenye, show moja kubwa ya asubuhi kwa jina #DAMKA !!

Mjue Alex Yang!!

Facebook : Alex Yang Muembu
Twitter : @alexmuembuh
Instagram :@alexmuembuh

Share:

0 comments:

GET NOTICED

GET NOTICED
PRESENTER ALI. Powered by Blogger.

Author Details

contact us



Translate

Labels